Ni mara nyingine tena
unakutana nasi katika toleo la 2 la “Kona ya PRO” la Juni 2014, likiwa
limesheheni mambo mbalimbali yahusuyo mchezo wa riadha (Athletics). Kona hii
hukujia kila mwezi ikiwa imekusanya masuala kadhaa.
Ninachukua nafasi hii,
kuipongeza serikali kwa juhudi zake katika kuinua riadha nchini Tanzania, mchezo
huu umekuwa katika kipindi cha mpito kwa miaka kadhaa huku changamoto
mbalimbali zikisababisha nchi ya Tanzania kutong’ara kimataifa kama ilivyokuwa
miaka ya 1960 hadi 1970.
Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania imekuwa ikijitahidi kwa udi na uvumba kutaka heshima ya
mchezo huu ilirudi, kwani kumekuwepo mwitikio mkubwa kwa viongozi kujitokeza
katika shughuli zinazohusu mchezo huu, wanapoalikwa kuhudhuria.
Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo imekuwa ikijitokeza kutoa msaada wa hali na mali
kwa ajili ya kufanikisha shughuli mbalimbali za riadha.
Pia suala la timu ya
taifa, serikali imejitokeza na kutoa msaada wa hali na mali kwa wanariadha
kuweka kambi ya mafunzo katika nchi za Uturuki, Kenya, Ethiopia, New Zealand na
China kwa ajili ya Michuano ya Jumuiya ya Madola (Commonwealth) mwezi Julai
nchini Scotland.
Ninaamini juhudi za
serikali kutaka kurudisha heshima yake kunaonekana dhahiri kwani Waziri wa
Mambo ya Nje wa Tanzania Bernard Membe aliwakabidhi Bendera ya Taifa wanariadha
hao walioondoka kwa ajili ya kujiandaa na michuano hiyo muhimu.
Nitoe wito tu kwa
watanzania kujitoa kwa dhati kuhakikisha mchezo huu unarudi katika nafasi yake,
na sio kuiachia serikali ya Tanzania tu kwani “kidole kimoja hakivunji chawa”.
Domician Genandi
Mkurugenzi
Holili Youth Athletics Club (HYAC)
Juni 2014.
ILIYOPITA BOFYA KIUNGO HIKI
No comments:
Post a Comment