“SURPRISE RIO!” ni kipengele kitakachokuwa kikikuletea matukio
ya kushangaza, kuchekesha, kuhuzunisha na wakati mwingine kukupanua ufahamu.
Leo nitamwangazia Lameck
Wambura Misiwa;
Machozi yanapotoka
huashiria furaha ama huzuni; ndivyo ilivyokuwa Desemba 8, 2013 kwa mwanariadha
Lameck Wambura Misiwa akiwa katika mbio za kilometa 5 Uhuru Marathon.
Uhuru Marathon 2013
zilimalizika kwa watanzania walau kuonyesha kwamba wanakuja vizuri katika
mchezo wa riadha ambao umeipa sifa Tanzania katika medani ya kimataifa licha ya
misukosuko mingi.
Kilometa 21 wanaume mtanzania Elia Daudi wa Holili Youth
Athletics Club alishika nafasi ya tatu akikimbia kwa muda wa saa 1:07.10, kwa
wanawake Jackline Sakilu aliiwakilisha vilivyo Tanzania kwa kushika nafasi ya
kwanza kwa muda wa saa1:15.25
Lameck Wambura alipotea
njia wakati akaiongoza kwa wanariadha wa mita 5000 kutoka na kuwa mgeni wa njia
za Jijini Dar es Salaam na kujikuta akiibukia Magomeni Mikumi akitarajia kuwa angekuwa
wa kwanza, aliposhtuka alirudi kwa njia nyingine na hadi viwanja vya Leaders
Club na kukuta washindi wa mbio hizo wakifurahi kwa kushika nafasi nzuri…aliangua kilio mwanariadha huyu kama inavyoonekana katika picha.
Miezi 5 baada ya tukio
hilo Lameck Wambura Misiwa alipatasafari ya kwenda Auckland, New Zealand kujiandaa na Michuano ya Jumuiya ya
Madola mwezi Julai mwaka huu Glasgow, Scotland.
Hakika “Lameck Wambura
is a Surprise of a Month”
ILIYOPITA
BOFYA KIUNGO HIKI
Imetayarishwa na:
Jabir Johnson, Afisa Habari na Mawasiliano
Holili Youth Athletics Club (HYAC)
Mei 2014.
No comments:
Post a Comment