HYAC

Attack with Style, Defend with Heart

Sunday 8 December 2013

WAMBURA RYOBA AANGUA KILIO UHURU MARATHON



*Apotea njia, atokea Magomeni
*Kurudi mshindi katangazwa
*Wanariadha wanyang’anyana maji
WAMBURA LAMECK RYOBA AKIANGUA KILIO MAPEMA LEO ASUBUHI
Mwanariadha Wambura Lameck Ryoba wa Holili Youth Athletics Club ameangua kilio baada ya kujikuta akishindwa kufanya vizuri licha ya kuliongoza kundi la wafukuza upepo baada ya kupotea njia kutokana na usimamizi mbovu wa mbio za Uhuru Marathon zilizofanyika Jumapili ya Desemba 8, mwaka huu.

Wambura akizingumza kwa masikitiko makubwa alisema kuwa alipotea njia kutokana na ukweli kwamba hakukuwa na vibao maalum vya kuonyesha njia za kupita katika mbio hizo za kilometa 5.

Aidha Mwanariadha huyo anayechipukia alisema amekasirishwa sana na waandaji wa mbio hizo kutokana na kutokuwa makini na wanariadha.

Pia Wambura alisema Waandaji wanapaswa kujipanga tena msimu ujao kwa ajili ya mbio hizo kutokana na changamoto ambazo zimejitokeza ikiwemo huduma ya maji kwa wachezaji haikuwa nzuri kwa mbio zote.

Uhuru Marathon imemalizika kwa Elia Daudi kutoka Arusha akimaliza katika nafasi ya 3 kwa kukimbia muda wa saa 1:07 akitanguliwa na wakenya wawili katika mbio za kilometa 21. 

Kwa upande wanawake Mtanzania Jackline Juma Sakili aliwainua watanzania baada ya kuongoza mbio hizo za kilometa 21 (Half Marathon)  kwa kukimbia saa 1:15:25

1 comment:

  1. Bwana Wambura pole sana kijana !! Hayo ndio mafunzo ya mchezo huu, tafadhari sana usikate tamaa, nina hakika kuwa utafinikiwa endelea na mazoezi na pia usikate taama kabisa kijana.

    ReplyDelete