HYAC

Attack with Style, Defend with Heart

Thursday 19 December 2013

HYAC YAJIPANGA KUONYESHA MAKUBWA MBIO ZA KARATU TEN-K



Wanariadha 6 wa Holili Youth Athletics Club wanatarajia kukimbia mbio za Karatu Ten – K zitakazofanyika Jumamaosi ya Desemba 21 mwaka huu.
NEEMA MATHIAS

Msemaji wa Holili Youth Athletics Club Johnson Jabir amewaambia waandishi habari kuwa wanawake watakuwa wawili ambao watakimbia kilometa 5.

Amewataja wanariadha hao wa kike kuwa ni Neema Mathias ambaye ana rekodi ya kukimbia mbio za Kilometa 21 za Serengeti Marathon na kushika nafasi ya 3 nyuma ya Furaha Sambeke na Mary Naali; na mwanamke mwingine ni Irene Asia.

Msemaji huo ameongeza kusema wanaume watakuwa 4 ambao ni Mapacha Francis Makombe na Richard Makombe, Wambura Lameck ambaye anashikilia rekodi ya pekee katika mbio za Uhuru Marathon mwaka huu na Nelson Priva.

Hata hivyo amesema Timu hiyo itaondoka kambini Tarakea Wilayani Rombo kesho mchana (Desemba 20, 2013) na kuwasili Kaaratu mkoani Arusha siku hiyo hiyo jioni ambapo itaongoza na Uongozi mzima wa timu hiyo pekee nchini Tanzania.

Viongozi watakaombatana na Timu hiyo ni Mkurugenzi Domician Genandi, Meneja wa Timu Nelson Mrashani na Katibu wa Timu Innocent Mushi.

Itakumbukwa kwamba Ushiriki wa Holili Youth Athletics Club ni muhimu mno hasa ikizingatiwa kuwa ina malengo ya kushiriki kila mbio kwa ajili ya kusaka vipaji na kuviinua.

No comments:

Post a Comment