HYAC

Attack with Style, Defend with Heart

Wednesday 11 December 2013

SAFARI YA KUTOKA BUNDA HADI LAMADI SERENGETI MARATHON 2013- SEHEMU YA 2



Serengeti Marathon zilianza mapema ya Desemba 4 mwaka huu katikati ya mbuga za Serengeti wilayani Bunda mkoani Mara kwa kufunguliwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Joshua Milumbe.
WANARIADHA KUTOKA BUSEGA, JOHN KABUTI, ALI JUMA NA ISSA JUMA WAKIWA KATIKA MBUGA ZA SERENGETI TAYARI KUANZA KUFUKUZA UPEPO.
Ambapo katika ufunguzi huo wanariadha zaidi ya 100 walihudhuria na kushuhudia mbio hizo zikianza ndani kidogo ya geti la Ndabaka yapata kilometa 3.5 kutoka barabara iendayo Musoma-Mwanza.

Muasisi wa Mbio hizo Dk. Titus Kamani alishiriki mbio hzio licha ya kwamba alikimbia kilometa 5 kwa uzinduzi na kushika nambari moja huku akishuhudiwa na washiriki wengine.

William Mwakilema, Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Serengeti ambayo imo katika maajabu makubwa hapa ulimwenguni alisema mbio hizo zinazidi kutia hamasa na kuendeleza vita dhidi ya wale wanaowinda wanyamapori pasipo kufuata taratibu na kanuni za wanayamapori.

Wanariadha watoto kutoka familia moja Issa Juma (14) anayesoma darasa la 5 na Ali Juma (12) anayesoma darasa la 4 mwingine wa nyumba ya jirani yao John Kabuti (13) anayesoma darasa la 3 walikimbia mbia za kilometa 5.
 
ULINZI ULIKUWEPO KATIKA MBIO HIZO HASA IKIZINGATIWA WANYAMAPORIKAMA SAWALA, PUNDAMILIA, KONGONI NA WENGINEO WALIKUWA KARIBU SANA.
WANARIADHA KUTOKA NDANI NA NJE YA NCHI WALISHIRIKI SERENGETI MARATHON
DK. TITUS KAMANI MUASISI WA SERENGETI MARATHON AKIZUNGUMZA JAMBO KATIKA UFUNGUZI WA MBIO HIZO.
MHIFADHI MKUU WA HIFADHI YA SERENGETI, WILLIAM MWAKILEMA AKIZUNGUMZA JAMBO PEMBENI NI JOSHUA MILUMBE MKUU WA WILAYA YA BUNDA.
WANARIADHA WA FULL MARATHON (KILOMETA 42) WALIANZA KUTIMUA MBIO HIZO
WANARIADHA WA MBIO ZA KATI (HALF MARATHON) WAKIFUATILIA KWA MAKINI MAELEKEZO, NAMBA 146 NI NEEMA MATHIAS WA KLABU YA HOLILI ALIYESHIKA NAFASI YA TATU KWA WANAWAKE PALE ALIPOKIMBIA KWA MUDA WA SAA1:30:23.
KUTOKA KUSHOTO, DK. TITUS KAMANI, JOSHUA MILUMBE NA WANARIADHA WATOTO TISHIO LA KESHO KABLA YA KUANZA KILOMETA 5

MTAYARISHAJI: JOHNSON JABIR

ITAENDELEA…

No comments:

Post a Comment