HYAC

Attack with Style, Defend with Heart

Friday 27 December 2013

JOHNSON JABIR ASHEHEREKEA KRISMAS NA FAMILIA YA GENANDI MJINI HOLILI

Kila mwaka unapofika mwezi Desemba, watu mbalimbali ulimwenguni pote, kila mmoja kwa tamaduni ya eneo analoishi huwepo shamrashamra, vifijo na nderemo.

http://3.bp.blogspot.com/-rxNICCiIcPg/UPKv8574-kI/AAAAAAAAiB4/2i4xYZ8eKOU/s640/jabir+johnson+1.JPG

JOHNSON JABIR
Nchini Tanzania watu wa jamaa, makabila mbalimbali huanza purukushani za kumaliza mwaka, mojawapo ikiwa ni maandalizi ya sherehe za Kuzaliwa kwa Yesu (Krismas) na Mwaka Mpya.

Waumini wa dini ya Kikristo huwa na shamrashamra zaidi ya wengine kutokana na ukweli kwamba sikukuu ya Krismas hupendwa sana kutokana na wao kumjua zaidi Kristo Yesu.

Desemba 2013, niliona vema nitue katika mji mdogo ulio maarufu sana nchini Tanzania, wa Holili. Huenda ni maarufu kutokana na sababu lukuki lakini moja kati hizo ni uwepo wa kituo cha mpaka kati ya Tanzania na Kenya.

Sio mara yangu ya kwanza kufika Holili, kwa mara ya kwanza ilikuwa Desemba 2012 nilipongia mkoani Kilimanjaro nikiwa na mwezi mmoja tulifika na rafiki yangu aliyefahamika kwa jina la Edward Haule.

Nilipofika hapo nilipokewa na familia moja maarufu sana mjini humo ya jamaa mmoja anafahamika kama Domician Genandi Rwezaura.

Ukifika hapo, ukiuliza “Domi” hakuna asiyemjua, mtoto hata mkubwa watakuambia na kukueleza anapoishi.

Nilistaajabu sana kukutana watu kadha wa kadha wakimfahamu huyu  anafahamika kwa jina la “Domi”.

Nikaamua kuwauliza nini hasa, wakaniambia kwamba Domi ni mfanyabiashara, licha ya kazi yake hiyo lakini kubwa zaidi ni mcheshi sana kwa watu wa eneo hilo tangu wameanza kufahamu kwani kuna wafanyabiashara wengi lakini iweje huyo pekee?

Nikafurahi sana kusikia maneno hayo ya faraja kutoka kwa watu wa eneo hilo.
 

NELSON MRASHANI, INNOCENT MUSHI NA DOMICIAN GENANDI
Desemba 23, 2013 alinipokea na kunipeleka katika eneo  mojawapo la biashara zake linalojulikana kwa jina la “KWETU PAZURI”.

Nikastaajabu kwa mara nyingine  kwanini panaitwa “KWETU PAZURI”  hasa nikikumbukwa waimbaji kutoka nchini Rwanda wa Christ Ambassadors waliowika na Albamu yao ya “KWETU PAZURI” miaka 2010.

Nikaambiwa hapo wengi wanapapenda kutokana na huduma nzuri wanazopata hapo ukilinganisha na mahali pengine mjini humo. Utakutana na vinywaji, vyakula vizuri na hata ukumbi wa kutazama mechi mbalimbali za soka kwa wale wapenda soka na filamu.

Nikala chakula kizuri, mimi ni mpenzi mno wa Wali Kuku na Soda nikafurahi kweli kwani kilikuwa kizuri hadi nikahisi hakuna haja ya kuondoka mapema ulimwenguni.

Baada ya hapo hali ya mambo ikaanza kuwa nzuri lakini Domi akanipa taarifa kwamba Desemba 26, 2013 angekuwa  sherehe ya binti yake Winny alikuwa akipata Komunyo katika Kanisa la Katoliki Sinai-Holili.

Krismas iliwadia waliamka na kwenda kanisani hapo hapo Holili, mimi siku hiyo sikwenda kabisa nilibaki nalala tu kutokana na kazi nzito nilizokuwa nikikamilisha siku ya nyuma.


Jioni yake tuliwajibika kwa miongoni mwa majirani aliyefahamika kwa jina la Kessy katika kusheherekea siku  hiyo , hakika ilikuwa ya kupendeza kuliko kawaida, tulikula, tukanywa vile tunavyovipenda hatimaye giza likaanza kulinyemelea anga ndipo nilipoondoka na kwenda kulala sehemu niliyofikia ya “Afrika Sana”.


WINFRIDA “WINNY” RWEZAURA
Nilipoamka tu nikamshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuiona Desemba 26 ndani ya taifa kubwa na zuri la Tanzania likiwa limejaa fursa nyingi za kuwekeza.

Ilikuwa ni Alhamis ya Desemba 26, ndugu, jamaa na marafiki walijumuika pamoja katika sherehe hizo kwa familia ya Domi.

Itakumbukwa kwamba Domi ni mzaliwa wa Kijiji cha Maziba mkoani Kagera (zamani Ziwa Magharibi) hivyo sikushangaa nilipokuwa nikisikia lafudhi za kutoka huko napo pia nilihisi kuwa sisi ni watanzania kweli kweli.

Nasema hivyo kwasababu, hakuna aliyeniuliza mimi ni kutoka kabila gani na mkoa gani nami nikaonekana miongoni mwa familia ya jamaa huyo ambaye hakika ni mcheshi. Utafurahi ukikaa naye!!

Winfrida “Winny” Rwezaura ni miongoni mwa watoto wa Domi wengine ni Karen “Kukugonza” na Genandi “Rwechungura” alizaliwa Agosti 17, 2003.

No comments:

Post a Comment