HYAC

Attack with Style, Defend with Heart

Saturday 7 December 2013

HOLILI YOUTH ATHLETICS CLUB YAWASILI DAR, UHURU MARATHON



*Wajigamba kufanya vizuri
*Dickson Marwa, Sambu Andrew wanatarajiwa kuwemo
* Flora Yuda aliibuka mshindi wa 4 Serengeti Marathon anatarajiwa kushiriki Half Marthon
Uhuru Marathon inatarajiwa kuanza kutimua mbio zake hapo kesho jumapili ya Desemba 8 mwaka huu ikiwa ni siku moja kabla ya maadhimisho ya miaka 52 ya uhuru wa Tanzania Bara.

Wakati hayo yakijiri Holili Youth Athletics Club (HYAC) ikiwa ni kalbu pekee nchini Tanzania inayojihusisha na riadha imethibitisha kuwasili kwa timu ya wakimbiza upepo akali ya 12 jioni ya leo Jijini Dar es Salaam.

Msemaji wa Klabu hiyo Johnson Jabir alisema timu ya wafukuza upepeo kutoka klabu hapo mkoani Kilimanajro imewasili majira ya saa 11 jioni leo Jumamosi ikitokea mkoani humo.

Hata hivyo HYAC imejigamba kufanya vizuri ikilinganishwa na Serengeti Marathon kutokana na ukweli kwamba hali ya hewa Jijini Dar es Salaam ni nzuri na wachezaji wengi wa klabu hiyo wamezoea kukimbia katika barabara za lami hivyo itakuwa kazi rahisi kwao kufanya vizuri.

Mbio hizo zinatarajiwa kuanza mnamo saa 12:30 katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.

Itakumbukwa kwamba Desemba 4 mwaka huu wanariadha 4  kutoka HYAC  walishiriki Serengeti Marathon iliyofanyika mkoani Mwanza ikianzia mkoani Mara katika Wilaya ya Bunda.

No comments:

Post a Comment