HYAC

Attack with Style, Defend with Heart

Friday 27 December 2013

HOLILI YOUTH ATHLETICS CLUB YAALIKWA ZANZIBAR JANUARI 12



HOLILI

Klabu pekee ya Riadha nchini Tanzania, Holili Youth Athletics Club (HYAC) ya Wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro inatarajiwa kushiriki Mashindano ya Riadha ya Sherehe za Mapinduzi kutimiza miaka 50 ya uhuru wa Visiwa hivyo.
MIONGONI MWA WANARIADHA WA HYAC WAKIWA KATIKA KARATU SPORTS FESTIVAL 2013
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Menejimenti ya Klabu hiyo ilisema Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Taifa Suleiman Ame Hamis aliwaandikia barua ya mwaliko yenye Kumbukumbu Na. CRT/Z/VOL II/IMU/1147 ya kuwataka kuhudhuria sherehe hizo.

Taarifa ya Menejimenti hiyo iliongeza kusema Chama cha Riadha Zanzibar (ZAAA) kimetaka kuandaa timu ya wanariadha wataokwenda kushiriki mbio hizo.

Hata hivyo ZAAA imewataka kujigharimia wenyewe kuelekea kufanikisha mbio hizo  maalum kabisa kwa ajili ya miaka 50 ya uhuru wa Zanzibar.

Akizungumza, Meneja wa Klabu Nelson Mrashani aliongeza kusema timu yake ipo tayari kutokana na ukweli kwamba wachezaji wake wapo kwenye Kambi Tarakea mpakani mwa Tanzania na Kenya hivyo ni suala la kuchagua idadi ya watakaokwenda kuwakilisha.

Hata hivyo alitanabaisha kuwa hawataweza kupeleka wanariadha wengi kutokana na ufinyu wa bajeti ya klabu hiyo hasa ikizingatiwa kwamba mpaka sasa haijapata wafadhili wowote kwa ajili ya kuwasaidia kufikia malengo.

Mkurugenzi wa Klabu hiyo Domician Genandi aliwataka wadau kote nchini kujitokeza kwa wingi kuunga mkono juhudi za kuinua riadha Tanzania kwa kutoa michango yao ya hali na mali katika klabu yake.

Aidha alitanabaisha kuwa HYAC imejipanga kuifikia mikoa yote nchini kwa ajili ya kuvumbua vipaji na hata safari ya Zanzibar ni muhimu kwao kwani vipaji vitakavyoonekana havitaachwa kamwe.

No comments:

Post a Comment