HYAC

Attack with Style, Defend with Heart

Sunday 1 December 2013

HOLILI YOUTH ATHLETICS CLUB KUTOA WANARIADHA 4, SERENGETI MARATHON DESEMBA 4



WANARIADHA wanne kutoka Holili Youth Athletics Club wanatarajiwa kushiriki Serengeti Marathon siku ya Jumatano Desemba 4 mwaka huu.
FURAHA SAMBEKE NA NELSON MRASHANI

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Klabu hiyo imesema wachezaji hao wanne wapo katika kambi yao iliyoko Tarakea Wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro.

Imewataja nyota hao kuwa ni Neema Mathias na Furaha Sambeke kwa mbio za wanawake huku Baraka William na Godfrey Charles kwa mbio za wanaume.

Taarifa ya klabu hiyo imeongeza kuwa wanariadha wake wataungana siku ya Jumatatu Desemba 2 mwaka huu na Wakenya kutoka Klabu ya Riadha iliyopo Machakos  wenye ushirikiano mkubwa na klabu hiyo katika mbio za Serengeti Marathon

Mpaka sasa Holili Youth Athletics Club ina jumla ya wanariadha 14 walioko kambini kujiandaa na michuano mbalimbali ya riadha kote ulimwengu.

  Wakiwa hapo huendelea na shughuli mbalimbali ikiwemo ya kutafuta kuni kwa ajili ya kupikia kama walivyokutwa na kamera yetu.





 



No comments:

Post a Comment