BELFAST MARATHON 2014
Mbio ndefu za Belfast, hufanyika kila mwaka katika Mji
wa Belfast, Kaskazini mwa Ireland. Belfast ni miongoni mwa miji mikubwa na
inayojulikana katika UK.
Belfast
Marathon hufanyika kila
Mei Mosi ambapo imegawanywa katika maeneo 5 tofauti, ambayo ni Wanaume,
Wanawake, Timu za riadha, Wakongwe wa mbio na Baiskeli za walemavu.
Belfast Marathon huratibiwa na Mamlaka
ya Jiji la Belfast na Chama cha Riadha cha Ireland ya Kaskazini.
Ilianza mwaka 1982, hadi mwaka 2012 ilikuwa imetimiza miaka 31
huku idadi ya washiriki ikiongezeka ambapo mwaka 2011 walifikia washiriki zaidi
20,000.
Mshindi wa kwanza katika Belfast
Marathon kwa wanaume alikuwa Gregory Hannon aliyekimbia kwa muda wa saa
2:20:25.
Mkenya wa kwanza kuchukua taji hili kwa
wanaume alikuwa Joel Kipchumba katika Belfast Marathon 1991 alipokimbia kwa
muda wa saa 2:18:56.
Urga Negewo aliweka rekodi ya kuwa
mwanariadha wa kwanza kwa wanaume kutoka Ethiopia kunyakua taji hilo katika
Belfast Marathon 2010 alipokimbia kwa
muda wa saa 2:16:53.
Kwa wanawake Julia Myatt kutoka
Ethiopia alikuwa mwanamke wa kwanza kutwaa taji hilo katika Belfast Marathon
2004 alitumia muda wa saa 2:52:52; mkenya wa kwanza Joyce Kandia alitwaa taji
hilo mwaka 2006 akikimbia kwa muda wa saa 2:43:11.
Belfast Marathon 2014 ilifanyika na
kushuhudia Fredy Sittuk (Kenya) akitwaa taji hilo kwa wanaume akikimbia kwa
muda wa saa 2:18:30; kwa wanawake Bayrush Shiferaw (Ethiopia) aliibuka kidedea
akitumia muda wa saa 2:41:20.
LONDON MARATHON 2014
Ni mbio inayodhaminiwa na Virgin Money kwa sasa ambayo hukimbiwa
katika Jiji la London; ikiwa ni mbio ya pili kwa ukubwa katika UK, ikianzia ile
ya Great North Run.
April 13, 2014 ilikuwa ikitimiza miaka
34 tangu kuanzia kwake Machi 29. 1981, London Marathon itakuwa ikitimiza miaka
35 mwaka ujao na itafanyika April 26, 2015.
Mbio hii ilianzishwa na mkimbiaji wa
zamani wa Olimpiki na mwandishi habari Chris Brasher na mwanariadha kutoka
Wales John Disley, ikiwa ni miaka miwili baada ya kuanzishwa New York Marathon
1979.
Kwa sasa inaratibiwa na Hugh Brasher
(Mtoto wa kiume wa Chris Brasher) na Mkurugenzi Mtendaji akiwa ni Nick Bitel.
April 13, 2014 Wilson Kispang (Kenya)
kwa wanaume alitwaa taji hilo akitumia muda wa saa 2:04:29, akifuatiwa na
Mkenya Stanley Biwott aliyetumia muda wa saa 2:04:55
Mwingereza Mo Farah alishika nafasi ya 8
akikimbia kwa muda wa saa 2:08:21 huku Ryan Vail kutoka nchini Marekani
akishika nafasi ya 10 kwa muda wa saa 2:10:57
Kwa wanawake alikuwa ni Edna Kiplagat
(Kenya) akikimbia kwa muda wa saa 2:20:19 akifuatiwa na Mkenya Florence
Kiplagat akitumia muda wa saa 2:20:24
PARIS MARATHON 2014
Hujulikana kwa jina la Marathon International de Paris ikiwa ni
miongoni mwa tukio kubwa barani Ulaya ukiachana na zile mbio mbili kubwa barani
humo Berlin Marathon na London Marthon.
Kenneisa Bekele 2014
|
Ilianzishwa mwaka 1976, katika historia
ya mbio nchini Ufaransa Paris Marathon iliwahi kufanyika kwa mara ya kwanza
1896 ikiwa na washiriki 191, Mwingereza Len Hurst aliibuka na ushindi akitumia
muda wa saa 2:31:30.
Len Hurst alitwaa taji hilo tena mwaka
1900 akitumia muda wa saa 2:26:28, Mfaransa wa kwanza katika mbio hizo alikuwa
na Albert Charbonnel alinyakua taji la Tour de Paris Marathon mwaka 1899, 1902
na 1903.
Mwaka 1896 waliiga kutoka Athens nchini
Ugiriki walipokimbia umbali wa kilometa 40 baadaye kiwango kamili cha olimpiki
kilipopitishwa na kuwa kilometa 42.195 .
Jean-Pierre Eudier (France) alitwaa
taji hilo la kwanza mmwaka 1976 akikimbia kwa muda wa saa 2:20:57
Mwaka 1984 Paris Marathon ilianzishwa
mbio kwa upande wa wanawake mpaka sasa zikiendelea. Itakumbukwa kwamba, mwaka
1991 mbio hizi hazikufanyika kutoka na Vita ya Ghuba.
Cheyech 2014
|
Djibouti ilikuwa ni nchi ya kwanza
kutoka barani Afrika kutoa mshindi wa mbio hizo (wanaume) Paris Marathon 1984,
Ahmed Salah akikimbia kwa muda wa saa 2:11:58; Ahamed Salah alichukua tena
mwaka 1986 akitumia muda wa saa 2:12:44.
Kwa wanawake, Kenya ilikuwa nchi ya
kwanza kutoka barani Afrika kutoa mshindi katika Paris Marathon 2001, Florence
Borsosio akikimbia kwa muda wa saa 2:27:53.
Mwaka 2014, Kenenisa Bekele alikuwa
raia wa 5 (wanaume) kutoka nchini Ethiopia kutwaa taji hilo akikimbia kwa muda
wa saa 2:05:03 na kuweka rekodi ya kwanza ya juu katika mbio hizo ambayo
haikuwahi kufikiwa na mwanariadha yeyote tangu kuanzishwa kwake.
Washindi wengine kutoka Ethiopia
waliowahi kutwaa taji hilo, Ambese Tolossa 2004 (2:08:56),Gashaw Asfaw 2008
(2:08:03),Tsegay Kabede 2008 (2:06:40),Tadesse Tola 2010 (2:06:41).
Kwa wanawake katika Paris Marathon
2014, Mkenya Flora Cheyech alitwaa taji hilo akitumia muda wa 2:22:44 na kuwa
raia wa 6 kutoka nchini Kenya kwa wanawake kutwaa taji la mbio hizo.
ILIYOPITA
BOFYA KIUNGO HIKI
Imetayarishwa na:
Jabir Johnson, Afisa Habari na Mawasiliano
Holili Youth Athletics Club (HYAC)
Mei 2014.
No comments:
Post a Comment