Leo katika
kipengele hiki tutaangazia mwanariadha mkongwe nchini Tanzania John Stephen Akhwari na Michuano ya Olimpiki
nchini Mexico mwaka 1968.
JOHN STEPHEN
AKHWARI
Mwanariadha wa zamani John Stephen Akhwari, alizaliwa mwaka 1938 Mbulu,
Tanganyika sasa ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akhwari ni mwanariadha wa mbio ndefu, ambapo mwaka 1968 aliiwakilisha
Tanzania katika Michuano ya Olimpiki iliyofanyika Mexico City.
1968 Olympic
Marathon
John Akhwari alipokuwa akishiriki Mexico City, alipata mshtuko wa misuli
(ilisinyaa) kutokana na hali ya hewa ya huko iliyokuwa ya juu katika Jiji la
Mexico.
Akhwari hakuwahi kupata mazoezi katika Uwanda wa Juu alipokuwa nchini
Tanzania. Hadi kilometa 19 alikuwa mbele na wakimbiaji wengine na alikuwa
katika kiwango kizuri cha kumfanya ashinde lakini haikuwa hivyo.
Baada ya kupata matatizo hayo alifungwa bandeji katika goti, katika
jointi na begani. Hata hivyo aliendelea kukimbia, na kumaliza wa 57 na kuwa
miongoni mwa waliomaliza mbio hizo za kilometa 42.
Walianza wanariadha 75, mshindi alikuwa Mamo Wolde kutoka nchini Ethiopia
aliyekimbia kwa muda wa saa 2:20:26; Akhwari alimaliza kwa muda wa saa 3:25:27,
wakati kukiwa na watu wachache, maelfu ya watu wakitawanyika uwanjani hapo, na
jua likikaribia kuzama.
Warusha matangazo kwa njia ya runinga wakiwa tayari wameshaondoka, ndipo
neno likatoka katika vipaza sauti na spika zake kuwa kuna mshiriki mmoja
anakaribia kumaliza.
Alipomaliza mstari wa kumalizia kilometa 42, pongezi, vigelegele na
bashasha kutoka kwa hadhira ndogo vilimpokea.
Baadaye aliweza kuhojiwa na vyombo vya habari, kilichomfanya aendelee
kukimbia wakati akiwa na majeraha Akhwari alisema
“Nchi yangu haikunituma maili 5000 kuanza mbio, ilinituma maili 5,000
kumaliza mbio”.
Akhwari na
Riadha
Kabla ya Mbio za Mexico City Olympics 1968, Akhwari alikuwa amepambana
katika michuano mbalimbali. Alimaliza wa kwanza katika African Marathon
Championships.
Pia Akhwari alishika nafasi ya 5 katika Michuano ya Jumuiya ya Madola
1970 akikimbia kwa muda wa saa 2:15:05. Mshindi wa michuano hiyo alikimbia kwa
muda wa saa 2:09:28.
Mkongwe huyo katika Michuano ya Jumuiya ya Madola 1970 alikimbia mita
10,000 kwa muda wa dakika 28:44 akipitwa na mshindi wa kwanza kwa sekunde 30
tu.
Hakika John Stephen Akhwari alikuwa mwanariadha wa dunia kwa miaka ile ya
1960-1970.
Baada ya
kustaafu Riadha
Akhwari aliishi miaka mingi kijijini na familia yake, akiwa na mke mmoja
na watoto 6. Walikuwa wakilima mashamba kwa bidii zote hadi pale dunia
ilipotambua mchango wake katika riadha.
Pia aliamua kutumia jina lake kuanzisha taasisi inayoitwa John Stephen
Athletic Foundation; taasisi iliyojikita katika kufundisha wanariadha katika
michuano ya Olimpiki.
Mwaka 2000 alialikwa katika Michuano ya Olimpiki nchini Australia, pia
alionekana katika maandalizi ya Michuano ya Olimpiki mwaka 2008 Jijini Beijing
akiwa kama Balozi wa kujitolea.
Aprili 13, 2008 alikuwa miongoni wa waliokimbiza Mwenge wa Olimpiki
Jijini Dar es Salaam aliyeiwakilisha Tanzania nchini hapa.
Holili Youth Athletics Club (HYAC) ilikutana naye Desemba 22, 2013 katika
Tamasha la Michezo la Karatu (Karatu Sports Festival) lililofanyika Karatu
mkoani Arusha.
ILIYOPITA
BOFYA KIUNGO HIKI
Imetayarishwa na:
Jabir Johnson, Afisa Habari na Mawasiliano
Holili Youth Athletics Club (HYAC)
Mei 2014.
No comments:
Post a Comment