HYAC

Attack with Style, Defend with Heart

Sunday 26 October 2014

ADELINA AUDAX ATWAA USHINDI WA TATU ROCK CITY MARATHON 2014



 Adelina Audax, Mshindi wa tatu kutoka Holili Youth Athletics Club (HYAC) akipokea zawadi yake baada ya kufukuza upepo kilometa 21 Rock City Marathon 2014 jana Jijini Mwanza. ( Picha na Jabir Johnson)
Holili Youth Athletics Club iliendeleza rekodi yake ya kukaa katika nafasi nzuri katika mbio za Rock City Marathon zilizofanyika leo Jijini Mwanza ambapo kwa upande wa wanaume kilometa 21, Alphonce Felix alishika nafasi ya saba akitumia saa 1:03.45, Deo Hazard akionyesha uwezo tena akitumia saa 1:03.48 akiwa nafasi ya nane, Pascal Mombo akishika nafasi ya 10 akitumia saa 1:04.35
Aidha wanariadha wengine kutoka klabuni hapo Josephat Joswa alishika nafasi ya 15 akifuatana kwa karibu kabisa na Lameck Misiwa nafasi ya 16 huku Elibariki Buko akishika nafasi ya 23.

Kwa upande wa wanawake Adelina Audax akishika nafasi ya tatu kwa saa 1:23.01, Furaha Sabaha nafasi ya sita akitumia saa 1:26.03 na nafasi ya tisa ikiwekwa na Neema Mathias licha ya kushtuka nyonga alifukuza upepo kwa saa 1:44.53
 
Kwenye mbio fupi Holili Youth iliwakilishwa na Pascalina Silvesta aliyekimbia mita 400 na kushika nafasi ya tatu akitumia dakika 1:07.40 huku akifanya vizuri katika mita 1500 ambako alitwaa taji hilo akitumia dakika 5:58.13

No comments:

Post a Comment