HYAC

Attack with Style, Defend with Heart

Monday 23 June 2014

KONA YA PRO: JUNI 2014 UTANGULIZI



UTANGULIZI
Ni mara nyingine tena unakutana nasi katika toleo la 2 la “Kona ya PRO” la Juni 2014, likiwa limesheheni mambo mbalimbali yahusuyo mchezo wa riadha (Athletics). Kona hii hukujia kila mwezi ikiwa imekusanya masuala kadhaa.

Ninachukua nafasi hii, kuipongeza serikali kwa juhudi zake katika kuinua riadha nchini Tanzania, mchezo huu umekuwa katika kipindi cha mpito kwa miaka kadhaa huku changamoto mbalimbali zikisababisha nchi ya Tanzania kutong’ara kimataifa kama ilivyokuwa miaka ya 1960 hadi 1970.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikijitahidi kwa udi na uvumba kutaka heshima ya mchezo huu ilirudi, kwani kumekuwepo mwitikio mkubwa kwa viongozi kujitokeza katika shughuli zinazohusu mchezo huu, wanapoalikwa kuhudhuria.

Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imekuwa ikijitokeza kutoa msaada wa hali na mali kwa ajili ya kufanikisha shughuli mbalimbali za riadha.

Pia suala la timu ya taifa, serikali imejitokeza na kutoa msaada wa hali na mali kwa wanariadha kuweka kambi ya mafunzo katika nchi za Uturuki, Kenya, Ethiopia, New Zealand na China kwa ajili ya Michuano ya Jumuiya ya Madola (Commonwealth) mwezi Julai nchini Scotland.

Ninaamini juhudi za serikali kutaka kurudisha heshima yake kunaonekana dhahiri kwani Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Bernard Membe aliwakabidhi Bendera ya Taifa wanariadha hao walioondoka kwa ajili ya kujiandaa na michuano hiyo muhimu.

Nitoe wito tu kwa watanzania kujitoa kwa dhati kuhakikisha mchezo huu unarudi katika nafasi yake, na sio kuiachia serikali ya Tanzania tu kwani “kidole kimoja hakivunji chawa”.

Domician Genandi
Mkurugenzi
Holili Youth Athletics Club (HYAC)
Juni 2014.


ILIYOPITA BOFYA KIUNGO HIKI



No comments:

Post a Comment