HYAC

Attack with Style, Defend with Heart

Monday 23 June 2014

KONA YA PRO: JUNI 2014, SUPRISE RIO



“SURPRISE RIO!” ni kipengele kitakachokuwa kikikuletea matukio ya kushangaza, kuchekesha, kuhuzunisha na wakati mwingine kukupanua ufahamu.

Leo nitamwangazia Lameck Wambura Misiwa;


Machozi yanapotoka huashiria furaha ama huzuni; ndivyo ilivyokuwa Desemba 8, 2013 kwa mwanariadha Lameck Wambura Misiwa akiwa katika mbio za kilometa 5 Uhuru Marathon.

Uhuru Marathon 2013 zilimalizika kwa watanzania walau kuonyesha kwamba wanakuja vizuri katika mchezo wa riadha ambao umeipa sifa Tanzania katika medani ya kimataifa licha ya misukosuko mingi. 

Kilometa 21 wanaume mtanzania Elia Daudi wa Holili Youth Athletics Club alishika nafasi ya tatu akikimbia kwa muda wa saa 1:07.10, kwa wanawake Jackline Sakilu aliiwakilisha vilivyo Tanzania kwa kushika nafasi ya kwanza kwa muda wa saa1:15.25

Lameck Wambura alipotea njia wakati akaiongoza kwa wanariadha wa mita 5000 kutoka na kuwa mgeni wa njia za Jijini Dar es Salaam na kujikuta akiibukia Magomeni Mikumi akitarajia kuwa angekuwa wa kwanza, aliposhtuka alirudi kwa njia nyingine na hadi viwanja vya Leaders Club na kukuta washindi wa mbio hizo wakifurahi kwa kushika nafasi nzuri…aliangua kilio mwanariadha huyu kama inavyoonekana katika picha.

Miezi 5 baada ya tukio hilo Lameck Wambura  Misiwa alipatasafari ya kwenda Auckland, New Zealand kujiandaa na Michuano ya Jumuiya ya Madola mwezi Julai mwaka huu Glasgow, Scotland.

Hakika “Lameck Wambura is a Surprise of a Month” 

ILIYOPITA BOFYA KIUNGO HIKI
Imetayarishwa na:
Jabir Johnson, Afisa Habari na Mawasiliano
Holili Youth Athletics Club (HYAC)
Mei 2014.

No comments:

Post a Comment