HYAC

Attack with Style, Defend with Heart

Thursday 26 June 2014

LAMECK MISIWA AIMWAGIA SIFA HYAC, AFUZU MBIO ZA DUNIA "JUNIOR" NCHINI MAREKANI



Lameck Wambura katika barua yake pepe kwa klabu ya Holili Youth Athletics Club ameyasema haya:

Habari za Tz ,wazima!
Mimi naendelea vizuri  nimefurahi sana kuona vijana wenzangu  wamepata ushindi Bagamoyo Historical Marathon, na mimi huku nitakuwa na ushindani wa cross- country ya  Oceania Juni 29, 2014. 

Mniombee  nadhani naweza  kuenda Uingereza  kwenye mashindano ya dunia ya Junior  na  Marekani, Hivyo Jumuiya ya Madola sitakwenda kwasababu ya mbio hizo mbili.

Napenda kuwapa wenzangu hamasa na  kuwakilisha klabu yetu ya HYAC.  

Nimeshafuzu  mita 5000  dk 14:15. pamoja na mita 3000.

Nawatakia mandalizi mazuri ya  mashindano ya taifa tutakuwa pamoja  nadhan kama mambo hayatabadilika. tutarudi tarehe 5/7/2014.

Ndimi,
 Lameck Misiwa.

No comments:

Post a Comment